Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL BLOG
Viewing all 1545 articles
Browse latest View live

Mshindi wa Big Brother Idris Sultan Atuhumiwa Kuvaa Saa Feki na Kuringishia Watu Mtandaoni...

$
0
0
Page maarufu ya Fake Watch Busta kutoka Mtandao wa Instagram imeibuka na tuhuma kuwa mshindi wa Big Brother Africa 2014 amevaa saa feki , mtandao huo ambao kazi yake ni kuweka wazi mastaa wanaovaa saa feki umeandika haya na kuambatanisha picha hiyo hapo juu....
From @fakewatchbusta - Big Brother Africa winner @idrissultan with the worst fake Richard Mille skull i've ever seen  Skull has meth teeth and ate too much  That Hublot is missing some gold paint on the lugs as well

50 Cent Admits That He Lied About Owning a Home in Africa....

$
0
0
Remember when 50 Cent boasted that he was almost done with building a home in Africa (he never said where in Africa) and said he was going to have the craziest house warming party ever? Well, he has admitted that he lied.

According to TMZ, 50 Cent filed legal documents in his bankruptcy case stating that he neither owns nor ever owned any real estate property in Africa. He's trying to prove to the courts that his lavish lifestyle is fake.

Kasi ya Magufuli Yamkuna Rais wa Rwanda Paul Kagame...Aamua Kumuiga Kwa Kufanya Hili Kwa Viongozi wa Umma

$
0
0
Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema kuwa atapunguza safari za nje za watumishi wa umma. Apongeza hatua anazochukua Rais Magufuli. 

Ameyasema hayo Jana wakati wa akiwahutubia viongozi mbalimbali wa Serikali yake 

KIMENUKA Tena Pemba...Kituo cha Afya, Maskani ya CCM na Nyumba za Wananchi Zateketezwa Kwa Moto...

$
0
0
Zikiwa zimebakia siku saba kufanyika marudio ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, kumejitokeza viasharia vya uvunjifu wa amani kwa kuharibiwa majengo ya Serikali na nyumba za watu binafsi.

Usiku wa kuamkia jana, Kituo cha Afya cha Kiuyu Minungwini, Maskani ya CCM Junguni pamoja na nyumba za wananchi katika maeneo ya Kangagani, Makangale, Msuka, Tumbe na Shumba, zimeteketezwa kwa moto na watu wasiofahamika.

Akizungumza kwa nyakati tofauti alipotembelea waathirika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud mohamed alilaani kitendo hicho.

Alisema kinachoonekana, hujuma hizo zinapangwa na watu wasioitakia mema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kwa lengo la kutaka kuwajengea hofu wananchi, nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa marudio, Machi 20.

Hata hivyo, aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama, itachukua hatua za haraka ili kuwabaini wote waliohusika na hujuma hiyo.

“Hivi ni vitendo vya makusudi, haiwezekani matukio hayo yote yatokee siku moja katika maeneo tofauti na kwa wakati mmoja, tutahakikisha wahusika tunawasaka na kuwafikisha mahakamani,” alisema.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Omar Khamis Othman ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza doria ili kuhakikisha amani na utulivu unadumishwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir Ali aliahidi kuwasaka na kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika kwa matukio hayo.

Alitoa rai kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa za watu wanaowatilia shaka katika maeneo yao.

“Tusiwaonee haya hawa watu, wanachangia kurudisha nyuma maendeleo yenu, mkiwaficha mtakuwa mnajiumiza wenyewe,” alisema kamanda huyo.

Mastaa wa Muziki Diamond Platnumz na Fid Q Watakiwa Kurudi Mikoani Kwao Kuokoa Jahazi.....

$
0
0

Staa wa muziki nchini Naseeb Abdul Juma a.k.a Diamond Platnumz ametakiwa kutoka Jijini Dar es salaam na kurejea Mkoani Kigoma alikozaliwa, ili kuwasaidia Wasanii chipukizi katika Mkoa huo.

Mbali na Diamond, Staa mwingine alietajwa ili atoke Jijini Dar es salaam na Kurejea Mkoani kwake ni Farid Kubanda a.k.a Fid Q, ambae ametakiwa kurejea Jijini Mwanza ili kusaidia kuukuza muziki wa Mwanza.

Mbali hao mastaa hao ambao wametajwa live majina yao, pia mastaa wote waliohamishia shughuli zao za sanaa Jijini Dar es salaam wametakiwa kurejea katika Mikoa yao ili kuondoa mrundikano wa wasanii katika Jiji hilo.

Hayo yalisemwa juzi ijumaa Jijini Mwanza na Msanii Chipukizi Joseph Stanford a.k.a Rich4D, katika hafla ya kumpongeza kwa ushujaa wake wa kutembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam, kwa ajili ya Kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutambua mchango wa wasanii nchini na kuwajumuisha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

"Wasanii wakubwa watoke Jijini Dar na warudi Mikoani kwao ili wawasaidie wasanii chipukizi wa Mikoani. Diamond arudi Kigoma. Fid Q arudi Mwanza. Hii itaondoa mrundikano wa wasanii wakubwa Dar na hivyo kupeleka fursa za sanaa mikoani". Alisema Rich4D.

Matembezi ya Miguu ya Msanii Rich4D yalianza Januari 16,2016 yakihusisha mikoa minane sawa na Kilomita 1,200 na yalifikia tamati Februari 10,2016, lakini adhma yake ya kuonana na rais haikuweza kutimia baada ya rais kuwa katika majukumu mengine ya kitaifa ambapo aliekuwa Katibu Mkuu Ombeni Sefue aliahidi msanii huyo kuonana na rais.

Wadau mbalimbali waliosaidia kufanikisha matembezi hayo akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana Raphael Shilatu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula, wameyapongeza matembezi hayo na kusema kuwa ni ya kizalendo ambapo wamemuomba Katibu Mkuu Mpya, Mhandisi John Kijazi kuhakikisha ahadi aliyoiacha Sefue inatimia ili msanii Rich4D afanikiwe kuonana na rais magufuli.
Staa Fid Q
Msanii Rich4D anaechipukia kwa kasi Jijini Mwanza ambapo tayari anatamba na ngoma mbili ambazo ni "Tawile" na "Huniwezi".
                  

JIPU la Uchaguzi wa Meya Jijini Dar es Salaam....Waziri Atoa Amri Uchaguzi Uwe Umefanyika Kabla ya Tarehe Hii....

$
0
0
Hatimaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene amemaliza mzozo wa uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kuagiza ufanyike kabla ya Machi 25 na kutaja sifa za wapigakura.

Uamuzi huo wa kutangaza tarehe na sifa za wapigakura unaonekana kuwa ahueni kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambavyo vilifurahia hatua kama hiyo, lakini wadau wa CCM wakafungua kesi iliyosababisha uchaguzi huo uahirishwe mara tatu.

Simbachawene, ambaye aliwahi kuagiza uchaguzi huo ufanyike kabla ya Februari 29 lakini ukakwama mara tatu, aliwaambia waandishi wa habari jana mjini hapa kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia kifungu cha 13 (1) cha Kanuni za Kudumu za Jiji.

Alisema watakaopiga kura katika uchaguzi huo ni madiwani wote wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni, wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wa viti maalumu ambao mchakato wa kuwapata ulianzia kwenye mamlaka za halmashauri hizo.

Simbachawene alisema wapigakura wengine watakuwa ni wabunge wa kuteuliwa na Rais, ambao ni Dk Philip Mpango, Balozi Agustine Mahiga, Dk Ackson Tulia, Profesa Joyce Ndalichako, Dk Abdallah Possi, Profesa Makame Mbarawa ambao ni wakazi wa jijini Dar es Salaam.

“Tunaomba vyama kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kukubali matokeo ili kutosimamisha maendeleo ya jiji la Dar es Salaam,” alisema.



Breaking News: Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Wakuu wa Mikoa 26....Kati Yao 13 ni Wapya, 7 Wamebakizwa na 5 Wamehamishwa

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.

Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
 
Wakuu wa Mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
  1. Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  2. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
  3. Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
  4. Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
  5. Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
  6. Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
  7. Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  8. Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
  9. Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
  10. Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
  11. Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
  12. Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
  13. Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  14. Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
  15. Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
  16. Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
  17. Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
  18. Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
  19. Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  20. Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
  21. Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
  22. Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
  23. Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
  24. Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
  25. Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
  26. Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016

Paul Makonda Aula..Apewa Ukuu wa Mkoa Dar es Salaam..Uteuzi wake Umekuwa Gumzo

$
0
0

Juhudi za Paul Makonda zaonekana kwa Rais Magufuli...Apewa Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.....Uteuzi wake wawa Gumzo mitandaoni watu mbali mbali wakimpongeza

Lulu: Hakuna Ushirikina Kwenye Ushindi Wangu....Adai Toka Utoto wake yeye Amekuwa Mwigizaji

$
0
0
Lulu amesema kuwa haamini ushirikina wala hajawahi kufanya kazi yoyote katika ushirikina kuanzia utoto wake.

Amefunguka hayo usiku wa kuamkia jana kupitia Friday Night Live ya EATV na EA Radio baada ya kuulizwa kuhusiana na comment zinazo endelea kwenye mitandao ya kijamii kuwa ushindi wa tuzo yake umetokana na ushirikina.

Lulu alifunguka kuwa kuanzia utoto wake amekuwa akiishi katika maisha ya uigizaji hivyo kila kitu kimepangwa na ndiyo maana amefanikiwa kufika hapo alipo.

Lulu ameiambia FNL “watu kama hawapendi maendeleo yako ni lazima wataongea lolote kuhakikisha kuwa wanakusema tu pale unapo fanikiwa”.

Hata hivyo msanii huyo aliamua pia kufungukia kuhusiana na mahusiano yake na mama mzazi wa marehemu Kanumba baada ya mama huyo kutoonekana kwenye kumpokea msani huyo ilihali mama huyo amehusika kwenye filamu iliyo mpa Lulu ushindi huo.

Lulu amesema hana tofautioi yoyote na mama huyo bali inawezekana alitingwa na shughuli za kimaisha na ndiyo maana hakuweza kwenda kumpokea uwanja wa ndege wa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Hataivyo alisema huwa wanawasiliana naye kwa simu japokuwa sio mara kwa mara.

Kuhusu uwepo wa mahusiano ya kimapenzi kati yake na Majay, Lulu alisema hawezi kuongelea suala hilo kwa kuwa bado mambo hayajafikia hatua nzuri.

“Siwezi kusema lolote kwa kuwa naweza kusema kuwa ni kweli, lakini ikawa si kweli na pia naweza kusema si kweli na ikawa kweli ” Alisema Lulu.

Mr. Nice Alitumwa na Mungu Kuja Kuninyanyua Mimi - Wabogojo Afunguka

$
0
0
Wabogojo amesema Mr. Nice ndiye alimtoa kwenye na kumfanya kuanza kujulikana kwa watu, hivyo kwake ni sawa na bosi wake na kila akirudi hapa nchini lazima aende nyumbani kwake kujua anaendeleaje na shughuli zake.

"Mr. Nice ndio bosi wangu, Mr. Nice ndio ambaye alifanya Watanzania, Wakenya, Wauganda na mataifa mbali mbali wakanitambua mimi, Mwenyezi Mungu alimtumia Mr. Nice kuninyanyua mimi, hata kama labda sijapata pesa nyingi sana kipindi niko na Mr. Nice lakini kitu nilichokipata kutoka kwa Mr. Nice ni zaidi ya fedha hata mi mwenyewe namwambiaga, ndio maana mpaka sasa hivi yule jamaa namuheshimu, kila nikirudi lazima niwasiliane nae na naendaga mpaka kwao", alisema Wabogojo ambaye pia ni kaka wa msanii wa bongo movies Shamsa Ford.

Pamoja na hayo akielezea changamoto ya kufanya sanaa nje ya nchi yake, wabogojo amesema alikuwa anapata shida siku za mwanzoni kutokana na lugha ya Kiswahili aliyokuwa akitumia, kushindwa kuwasiliana na watu wa jamii ya huko.

"Changamoto kubwa ilikuwa, lugha sisi ni waswahili hata shule hatutumii english, unaenda supermarket kununua lotion unanunua sabuni, tulikuwa tunajifunza pia kuishi mazingiraya kule", alisema Wabogojo.

Nimekasirika Kupata Hii Tuzo Kutoka Nigeria - Richie Afunguka Adai Alitaka zote Mbili

$
0
0
Richie ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Weekend Breakfast siku ya jumapili,, na kusema kuwa baada ya filamu yake kuingia kwenye hizo category mbili aliamini yeye anaweza hivyo alitaka ashinde zote mbili, ingawa kwenye tuzo za Tanzania haikuwahi kuwa nominated.

“Ningechukua zote mbili, nilipochukua ile moja nilikasirika, naamini kama ninajua, tuzo za Tanzania haikupita hata kuwa nominated, nilikwenda Nigeria nikiwa na uhakika ninaenda kushinda”, alisema Richie.

Pamoja na hayo Richie amesema sio mtu wa majivuno na kujionyesha kama ilivyo kwa wengine, kwani tuzo hiyo sio ya kwanza kuchukua, kwani alishawahi kuchukua tuzo kubwa zaidi ya hiyo mwaka 2001, pamoja na uvumilivu na bidii ndio umemfikisha hapo.

“Mi sio bishoo bishoo wa kujishaua, nilishawahi kushinda msanii bora wa kiume ya Mnet mwaka 2001, nina history kubwa sana, ukiangalia tangu nilipoanza nina miaka 18 ndio nachukua tuzo nyingine Nigeria, sasa mtu miaka miwili na nusu anataka awe na hela”, alisema Richie.

Pia Richie ameelezea mipango yake ya kufanya kazi na Bishanga ambaye ndiye alimtambulisha kwenye sanaa ya maigizo, na kusema iwapo atapa fursa atafanya naye kazi, kwani ka sasa yuko busy sana na majukumu ya kampuni yake.

“Bishanga yupo, nikiwa serious naweza nikafanya nae kazi, naweza nikampata jumamosi au jumapili, yuko busy sana, hata director wangu anapenda tufanye kazi na Bishanga na sababu zipo za msingi, lakini kama demand ipo basi ni suply tu itakayofuata”, alisema Richie.

Vile vile Richie amejibu tuhuma ambazo wasanii wengi wa filamu wanatuhumiwa kuwa baada ya kifo cha Steven Kanumba tasnia hiyo imeshuka ubora wake, na kusema kuwa tasnia hiyo haiwezi kushuka kwani kila siku wasanii wapya wanaibuka.

“Tasnia haijashuka, hata mimi nikiondoka haiwezi kushuka, tulikuwepo, wakaja wengine kina Kanumba, ni season na time, sio wivu na roho mbaya kwa nini kanumba, mimi Vicent Kigosi 'Ray' jina nilimpa mimi, nikasema utaitwa Ray, na pi nina dicpline”, alisema Richie.

Diamond Platnumz Amtumia Salamu za Pongezi PAUL Makonda Baada ya Kuteuliwa Kuwa Mkuu wa Mkoa...Asema Haya

$
0
0
Mwanamuziki Mwenye mafanikio makubwa katika mziki wa Bongo flava ametuma salamu za pongezi kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika haya:

Mafanikio hujaga kwa juhudi na kuto kukata tamaa... Hongera sana my brother @PaulMakonda kwa kuchaguliwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam... nakutakika kila lenye kheri kwenye kuhakikisha Dar es salaam yetu Inang'ara  @PaulMakonda 

Wafanyakazi Waliofukuzwa NIDA Wagoma Kupokea Barua Za Kuachishwa Kazi

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) waliofutiwa mikataba ya kazi, wamegoma kupokea barua za kuachishwa kazi wakidai kwamba hawajui kilichoandikwa kuhusu hatima ya madai yao.

Wafanyakazi hao walikutana jana Dar es Salaam na kiongozi wao, Seif Kibangu alisema wamekubaliana kutochukua barua hizo hadi pale watakapopata ushauri kutoka kwa wanasheria.

“Licha ya mishahara ya miezi mitatu tuna madai yetu mengine ikiwamo makato ya mafao yetu yaliyotakiwa kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, pia tumekuwa tukikatwa bima ya afya asilimia tatu ya mishahara yetu hatujui hatma yake.

"Sasa leo wanataka tuchukue barua hizo tena kwa kusaini kabla ya kujua kilichoandikwa hapana tuendelee kuvumilia haki yetu tutaipata,” alisema Kibangu.

Aliwakosoa waliochukua barua hizo akisema waliajiriwa kwa makundi, ingawa pia wapo waliopewa kazi hiyo kwa vimemo.

“Hili ni jasho letu, hatuibi cha mtu kwa hiyo tunastahili kupata haki zetu zote, mishahara tunayodai kwa miezi mitatu, acha hayo madai mengine... Tunadaiwa huko tunapoishi kwa kweli tunaomba wahusika waingilie kati jambo hili linatuumiza na kuyumbisha maisha yetu,” alisema.

 Akizungumza kwa niaba ya madereva wenzake, George Mmari alidai kuna gharama nyingi walizoingia ambazo Nida inapaswa kuzilipa ikiwamo malipo ya kuegesha na kuosha magari waliyokuwa wakiendesha.

Akizungumzia madai hayo, Ofisa Habari Mwandamizi wa Nida, Rose Mdami alieleza kushangazwa na hatua ya wafanyakazi hao kugoma kuchukua barua zao badala ya kuzipokea ili wajue kilichoandikwa ili kama wana madai waandike barua na kuyaorodhesha.

Haya Hapa Matokea ya Mechi ya Simba na Prison ya Mbeya Iliyochezwa Leo Jioni.....

$
0
0
Wakati watani zao wa jadi Yanga wamemaliza kucheza mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika dhidi ya APR ya Rwanda kwa ushindi wa goli 2-1 March 12, Simba wao wameshuka dimbani March 13 kuendeleza harakati zao za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Simba wameshuka dimbani kucheza dhidi ya klabu ya wajelajela wa Mbeya Tanzania Prisons, katika mchezo wao 23 wa Ligi Kuu Tanzania bara. Simba waliingia uwanjani kuhakikisha wanapata point tatu ili waendelee kuwa katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara.

Hata hivyo licha ya jitihada kubwa kuoneshwa ndani ya dimba la uwanja wa Taifa na Tanzania Prisons za kuataka kutoa sare, hazikuzaa matunda, kwani Simba ilifanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 kupitia kwa Awadh Juma dakika ya 88. Kwa matokeo hayo Simba anaendelea kuongoza Ligi akiwa na jumla ya point 54 akifutiwa na Yanga aliyemzidi point 3 na michezo miwili.

Nyota ya Mbwana Samatta Yazidi Kung'aa Genk...Afunga Goli Moja Kati ya Manne Waliyoshinda Usiku Huu zidi ya Oostende

$
0
0
Mbwana kafanya yake leo kaanza kipindi cha kwanza kafunga goal moja dakika ya 24 , Mpira Umeisha Muda si mrefu. Mechi ilikuwa kati ya Genk vs Oostende
Matokeo ya mwisho Genk 4 , Oostende 1


Tazama Hapa Video ya Goli la Mbwana Samatta Alilopachika Katika Mechi ya leo Kati ya KRC Genk na Oastende

$
0
0
Kwa mara ya kwanza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambayo inaongozwa na kocha lakini inachezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta, imempa nafasi ya kuanza katika mchezo wa leo dhidi ya klabu ya KV Oastende.

Samatta amepata nafasi hiyo ya kuanza mchezo wa leo March 13, ikiwa ni zaidi ya mechi nne amekuwa akiichezea timu hiyo akitokea benchi. Baada ya Samatta kuanza first eleven, alipachika  goli la kwanza kwa timu yake dakika ya 25 ya mchezo, lakini hilo pia ni goli lake la pili toka ajiunge na KRC Genk.

Samatta Mbwana Ally forward of Krc Genk looks behind him during the Jupiler Pro League match between Royal Mouscron Peruwelz and KRC Genk in the Le Canonnier Stadium in Mouscron, Belgium. *** MOUSCRON, BELGIUM - 06/02/2016  Photo by Nico Vereecken / Photonews ***

Goli la Samatta lilifuatiwa na neema kwa KRC Genk, kuibuka na ushidi wa goli 4-1, magoli ya KRC Genk yalifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 25, Balley dakika ya 39, Pozuelo dakika ya 81 na Camargo dakika ya 88, wakati goli la kufutia machozi kwa KV Oostende lilifungwa na Siani dakika ya 90.

Video ya goli la Samatta

Chanzo:Millard Ayo

Waajiri na Wadaiwa wa Mikopo ya Elimu ya Juu Wapewa siku 60.....HESLB yatoa namba za Mawasiliano

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatoa siku 60 kuanzia tarehe 14 Machi, 2016 kwa wanufaika wote wa mikopo wanaodaiwa na HESLB kujitokeza na kuanza kulipa madeni yao kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Aidha, katika muda huu wa siku 60 waajiri pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao wa kisheria wa kuwasilisha taarifa za waajiriwa wao waliohitimu katika vyuo vya elimu ya juu ndani na nje ya nchi. Taarifa zinazopaswa kuwasilishwa zijumuishe majina kamili ya waajiriwa, vyuo na mwaka waliohitimu.

Itakumbukwa kuwa Sheria iliyoanzisha HESLB (Sura 178) (kama ilivyorekebishwa) inatoa wajibu kwa mnufaika wa mikopo ya elimu ya juu na pia wajibu kwa mwajiri.

Wajibu wa Mwajiri
Hivyo basi, taarifa hii inalenga kuwakumbusha waajiri ambao bado hawatimizi wajibu wao kisheria (kifungu cha 20) wa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao wote ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu kwa HESLB ndani ya siku 28 tangu waajiriwe.

Adhabu ya kutotekeleza wajibu huu kwa mwajiri ni faini ya shilingi milioni saba (Tshs milioni 7) au kifungo au vyote kwa pamoja.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, baada ya HESLB kupokea orodha kutoka kwa mwajiri, itafanya uchambuzi ili kubaini wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu na kumwelekeza mwajiri kuingiza makato ya marejesho kwenye mshahara wa mnufaika na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB.

Adhabu ya kutowasilisha makato kwa HESLB ni faini ya asilimia 10 ya makato yote ambayo hayajawasilishwa na faini hii inapaswa kulipwa na mwajiri.

Wajibu wa mnufaika wa mkopo na wazazi, walezi, wadhamini
Aidha, pamoja na wajibu wa mwajiri kama ulivyofafanuliwa hapo juu, wanufaika wote wa mikopo ya elimu ya juu tangu mwaka 1994, wana wajibu wa kisheria (Kifungu cha 19 cha sheria ya HESLB), pamoja na mambo mengine, kuitaarifu HESLB kwa maandishi mahali alipo na kuandaa utaratibu wa kulipa deni lake la mkopo wa elimu ya juu.

Iwapo mnufaika wa mkopo atashindwa kutoa taarifa hizo, adhabu yake ni kushitakiwa mahakamani.
 
Aidha, HESLB inapenda kuwakumbusha wazazi, walezi na wadhamini wa wanafunzi walionufaika na mikopo kuwa wana wajibu wa kisheria (chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya HESLB) wa kuhakikisha kuwa taarifa muhimu za mnufaika waliyemdhamini zinaifikia HESLB.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, taarifa hizo ni pamoja na mahali alipo mnufaika, majina aliyotumia wakati akipata mkopo, mwajiri wake na kuhakikisha mnufaika aliyemdhamini anarejesha mkopo wake kwa HESLB.

Iwapo mwajiri, mnufaika au mdau yeyote ana swali, awasiliane na HESLB kwa simu zifuatazo: 0754 373481; 0763 459 165 au 022 2772432/33.

Lengo la HESLB ni kuhahakisha madeni yote yanakusanywa ili kuongeza uwezo wa kukopesha watanzania wengi zaidi. Ili kutekeleza hili, wanufaika, waajiri na wadau wengine wote wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kisheria ili HESLB itekeleze majukumu yake kama ilivyokusudiwa wakati ilipoanzishwa mwaka 2004.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

Mwisho
Imetolewa na:
Bw. Jerry Sabi,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji – HESLB
Dar es Salaam – Jumapili, Machi 13, 2016

Majibizano Makali kati ya Chris Brown na Ex wake Karrueche Tran yako Hapa

$
0
0
Chris Brown na Ex wa Karrueche Tran wamejibizana instagram hivi karibuni. Hii imetoakea baad aya CHris Brown kumtaja Karrueche Tran kwenye remix ya wimbo wake wa ‘Back To Sleep’.

LOWASSA na MBOWE Waongoza Mafuriko ya Kumtambulisha Katibu Mkuu Mpya wa CHADEMA Jijini Mwanza

$
0
0
Picha za awali za tambulisho wa Katibu mkuu wa CHADEMA Ndg Dr Vincent Mashinji uliofanyika leo jijini Mwanza mara baada ya hapo jana kuchaguliwa rasmi kuibba mikoba ya ukatibu mkuu wa CHADEMA iliyoachwa na aliyekuwa katibu mkuu DR SLAA.

Picha kamili za tukio hili zitakujia..




Nafasi za Kazi Equity for Tanzania Limited, Application Deadline 16th March, 2016

$
0
0
EQUITY FOR TANZANIA LIMITED (EFTA)
JOB VACANCIES

Organization

Equity for Tanzania Limited (EFTA) is an award-winning equipment finance company which provides equipment loans to small, medium and growing businesses in Tanzania.

Job Title: Internal Auditor (Moshi)

The Internal Auditor is responsible for ensuring that EFTA`s internal processes and procedures for risk management, internal control and corporate governance are effective and complied with. This includes ensuring that EFTA processes and procedures safeguard assets and reputation and enable good customer service.

Candidate specification

•    Experience: Prior internal or external audit experience.
•    Education Level: Degree in Financial or Business discipline from a reputable university. Member of professional accounting, internal audit or banking body (preferred)
•    Skills: Ms Office, Communication, report writing, analytic.

=======


Job Title: Finance Manager (Moshi)

The Finance Manager is overall responsible for financial processes and related recording for the head office as well as coordinating Branch Offices recording and reporting.

Candidate Specification

•    Experience: At least 5 years in financial accounting with at least 1year managing a team, experience working for one of the Big 4 will be a plus.
•    Education level: Accounting Degree from a reputable university.
•    Skills: Proficiency in MS Office (Particularly Excel) and accounting software is a must, excellent communication skills, careful attention to detail, ability to identify key issues and solutions.

=======


Job Title: Investment Officer (Morogoro/Mbeya)

The investment Officer will be directly responsible for dealing with EFTA customers, including attracting new customers, appraising applications for loans, and monitoring customers who have received loans. This is an excellent opportunity for motivated and energetic self-starters to secure challenging and rewarding roles with a multicultural rapidly growing company. There will be ample opportunity for career development and progression.

Candidate Specification

•    Experience: Prior bank lending or commercial business experience. At least 3 years if applying for the senior investment Officer Position. Experience in Agricultural lending is a plus.
•    Education level: Degree in financial or business discipline from a reputable university.
•    Skills: Ms Office, communication, driving, analytic.

========


Job Title: Book Keeper (Moshi/Arusha)

The Book Keeper will be responsible for recording day to day transactions of the branch and reporting to Head Office.

Candidate Specifications

•    Experience: at least 2 years in financial accounting/book keeping.
•    Education level: Accounting Degree from a reputable university
•    Skills: Proficiency in Ms Office (Particularly Excel) and accounting software is a must, excellent communication skills, careful attention to detail, ability to identify key issues and solutions.

=========


Job Title: Office Administrator (Moshi/Morogoro)

The Office Administrator will be responsible for day to day running of the office, Petty cash and dealing with customers.

Candidate Specifications

•    Experience: at least 2 years in a similar role.
•    Education level: Degree from a reputable University
•    Skills: Proficiency in Ms Office, excellent communication skills.

How to Apply

Send a cover letter and your C V to: sclarson@equityfortanzania.org with the subject “Internal Auditor Vacancy” or “Finance Manager Vacancy” or “Investment Officer Vacancy” or “Book Keeper Vacancy” or “Office Administrator Vacancy” by 16th March, 2016.


Source: Daily News 10th March, 2016
Viewing all 1545 articles
Browse latest View live