Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1545

Mwanamke Aibuka na Kusema 'Wema Niachie Bob Junior Wangu'

$
0
0
Jambo limezua jambo! Siku chache baada ya kuripotiwa kwa tukio la staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu kunaswa kimalovee na Rais wa Masharobaro, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, mwigizaji chipukizi, Bozi ameibuka na kudai ‘Wema niachie Bob Junior wangu’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mara baada ya habari hiyo kuruka hewani kupitia gazeti tumbo moja na hili, Amani la wiki iliyopita, mrembo huyo alipoziona picha za wawili hao alipoteza fahamu.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda huku akiangua kilio, Bozi alisema kuwa katika siku alizowahi kuumia ni siku hiyo alipoona Wema ametoka kwenye gazeti na mpenzi wake huyo.

Bozi alifunguka kwamba, alimbana Bob Junior kwa maswali lakini jamaa huyo hakutaka kumweka wazi kama yeye na Wema wanatoka.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1545

Trending Articles